UMOJA wa
wanamichezo waliowahi kucheza klabu mbalimbali zikiwemo za Ligi Kuu ya Soka
Tanzania Bara wenye maskani yao mjini Bukoba, Kagera, Bukoba Veteran Sports Club
ni katika kuhamasisha ushiriki wa timu za Tanzania, Kilimanjaro Stars na
Zanzibar Heroes, kwenye michuano ya Kombe la Tusker Challenge inayofanyika
jijini Kampala Uganda, umeandaa safari ya mashabiki walioko mkoani humo Kanda ya
Ziwa kwa ujumla kwenda kushangilia mechi za timu
hizo.Katibu Mkuu
wa Bukoba Veterans, Shijja Richard ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba kwa kuanzia,
mashabiki hao wataondoka mjini Bukoba Jumapili Novemba 25, 2012 kwenda
kuishangilia timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika mechi yake
ya kwanza ya michuano hiyo dhidi ya Sudan
Kaskazini.Amesema nia
na madhumuni ya safari hiyo ni kuhamasisha wachezaji wa timu za taifa za
Tanzania waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa kwenye ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati na kutoa hamasa kwa watanzania kujenga tabia ya
kushangilia timu zao na pia wanadhani kuwa ushiriki wao utaongeza ushindani
katika michuano hiyo.Amesema
tayari taratibu zote zimeshafanyika ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Shirikisho
la Soka la Tanzania (TFF) ili wawasiliane na mamlaka zinazohusika kwa ajili ya
kupatiwa eneo maalumu uwanjani litakalowezesha watanzania waweze kuishangilia
vizuri timu ya taifa.
“Tunatarajia
kwenda uwanjani na zaidi ya mashabiki 60 ambao hivi sasa wanakamilisha taratibu
za mwisho za kuvuka mpaka wa nchi. Matarajio yetu ni kuendelea kuziunga mkono
timu za taifa katika michuano hiyo hadi kufikia mwisho wa michuano. Tunaomba
watanzania wengine walioko kanda ya ziwa katika mikoa ya Shinyanga, Mara na
Mwanza watuunge mkono,”alisema Richard.Kikosi cha
kinatarajiwa kuwasili leo mjini Kampala, kikitokea Mwanza tayari kwa mashindano
hayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Tusker Challenge
2012 yanayotarajiwa kuanza kesho.Stars
imekuwa kambini mjini Mwanza kwa takriban wiki mbili sasa ikijifua vikali chini
ya kocha wake, Mdenmark Kim Poulsen kujiandaa kwenda kutwaa taji la nne la
Challenge.Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichopo kambini mjini
Mwanza, kinaundwa na makipa; Juma Kaseja
(Simba SC) na Deogratius Mushi ‘Dida’ wa Azam FC, mabeki; Kevin Yondan (Yanga),
Erasto Nyoni (Azam FC), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Shomari Kapombe na Amir
Maftah (Simba).
Viungo ni
Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan
Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo
(Yanga) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar) wakati washambuliaji ni John Bocco
‘Adebayor’ (Azam FC), Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba), Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu wa (TPM, DRC).Bara ambayo inajivunia kutwaa mara tatu Kombe la
Challenge katika miaka ya 1974, 1994 na 2010 na kushika nafasi ya pili mara
tano, imepangwa Kundi B pamoja na Sudan,
Burundi na Somalia.
Itaanza
kampeni zake Novemba 25 kwa kumenyana na Sudan saa 12:00 jioni, mchezo
utakaotanguliwa na mechi kati ya Burundi na Somalia itakayoanza saa 9:00 Alasiri
kabla ya kurudi tena dimbani, Novemba 28 kukipiga na Burundi, mchezo
utakaotanguliwa na mechi kati ya Somalia na
Sudan.Stars
iatahitimisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Somalia Desemba 1,
mchezo utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Sudan na Burundi. Mechi zote za
Stars zitakuwa saa 12:00 jioni.
MAKUNDI
RATIBA TUSKER CHALLENGE 2012:KUNDI A: Uganda, Kenya, Ethiopia na Sudan
Kusini
KUNDI B:
Tanzania, Sudan, Burundi na Somalia
KUNDI C:
Malawi, Eritrea, Rwanda na Zanzibar
RATIB KUNDI
A:Novemba 24,
2012:
Ethiopia v
Sudan (Saa 9:00 Alasiri)Uganda v
Kenya (Saa 12:00
jioni)Novemba 27,
2012:
Sudan Kusini
v Kenya (Saa 9:00 Alasiri)Uganda v
Ethiopia (Saa 12:00
jioni)Novemba 30,
2012:
Kenya v
Ethiopia (Saa 9:00 Alasiri)Sudan Kusini
v Uganda (Saa 12:00 jioni)
RATIBA KUNDI
B:Novemba 25,
2012:
Burundi v
Somalia (Saa 9:00 Alasiri)Tanzania v
Sudan (Saa 12:00
jioni)Novemba 28,
2012:
Somalia v
Sudan (Saa 9:00 Alasiri)Tanzania v
Burundi (Saa 12:00
jioni)Desemba 1,
2012:
Sudan v
Burundi (Saa 9:00 Alasiri)Somalia v
Tanzania (Saa 12:00
jioni)
RATIBA KUNDI
C:Novemba 26,
2012:
Zanzibar v
Eritrea (Saa 9:00 Alasiri)Rwanda v
Malawi (Saa 12:00 jioni)Novemba 29,
2012:
Malawi v
Eritrea (Saa 9:00 Alasiri)Rwanda v
Zanzibar (Saa 12:00
jioni)Desemba 1,
2012:
Malawi v
Zanzibar (Saa 9:00 Alasiri)Eritrea v
Rwanda (Saa 12:00
jioni)
ROBO
FAINALI:Desemba 3, 2012Mshindi
Kundi C vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa 10:00
jioni)Mshindi
Kundi A vs Mshindi wa Tatu Bora wa pili (Saa 1:00
usiku)Desemba 4, 2012 (16:00):
Mshindi
Kundi B vs Mshindi wa Tatu Bora wa kwanza (Saa 10:00
jioni)Mshindi wa
Pili Kundi A vs Mshindi wa Pili Kundi C (Saa 1:00
usiku)
NUSU
FAINALI:
Desemba 6,
2012Nusu Fainali
ya Kwanza (Saa 10:00 jioni)Nusu Fainali
ya Pili (Saa 1:00
usiku)
MSHINDI WA
TATU:
Desemba 8, 2012Waliofungwa
Nusu Fanali (Saa 10:00 jioni)
FAINALI:
Desemba 8, 2012Walioshinda
Nusu Fainali (Saa 1:00 usiku)
x
No comments:
Post a Comment