NEWS

BLOG

NEWS

Monday, November 26, 2012


KATIKA kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga ya Dar es Salaam inatarajia kwenda kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki mapema mwakani.Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kwamba ziara hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya Desemba na Februari 25, mwakani.Alisema pendekezo la kambi hiyo lilitolewa na kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts ambaye ana uzoefu na nchi hiyo ambayo ina vitu vinavyostahili kwa ajili ya timu kuweka kambi.Alisema ikiwa huko timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi mbili za kitrafiki na timu zitkazotajwa baadaye.Aidha, kocha mkuu wa timu hiyo amewapandisha wachezaji watatu wa kikosi cha vijana chini ya  miaka 20 wakiwemo kipa, Yussuf Abdallah, George Banda na Rehan Kibinga.Katika hatua nyingine, Bin Kleb aliasema wanajivunia uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Manji, kwani timu imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame, kufanya vema katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ambao ulimalizika kwa timu  kuongoza.Alisema kufanya vizuri katika Ligi Kuu, ni matunda ya timu hiyo kuweka kambi nchini Rwanda baada ya Kombe la Kagame

ZANZIBAR HEROES YAANZA DROO KATIKA MASHINNDANO  YA CHALLENGE CUP.
ZANZIBAR HEROES YAANZA DROO KATIKA MASHINNDANO  YA CHALLENGE CUP.
TIMU YA RWNANDA ILIYOKO KATIKA  MASHINDANO LEO  IMEWEZA KUIBUKA NA USHINDI WA MABAO2-0,MAGOLI ALIYEFUNGA NI MSHAMBULIAJI WA, WA TIMU YA YOUNG AFRICAN SPORT CLUB NIYONZIMA DAKIKA 79.
TIMU YA RWNANDA ILIYOKO KATIKA  MASHINDANO LEO  IMEWEZA KUIBUKA NA USHINDI WA MABAO2-0,MAGOLI ALIYEFUNGA NI MSHAMBULIAJI WA, WA TIMU YA YOUNG AFRICAN SPORT CLUB NIYONZIMA DAKIKA79

Sunday, November 25, 2012


PICHA ZA TAIFA STARS  NA SUDAN KATIKA UWANJA WA KAMPALA UGANDA, LEO TIMU YA TAIFA STARS IMEIBUKA NA USHINDI WA MABAO2-0,YAKIWEKWA NA JOHN BOCCO, MRISHO NGASA AKIWA ANATOA KROSI NA PASI.


JOHN BOCCO,NDIYE ALIYEFUNGA MAGOLI YOTE2-0.
MSUVA AKIMTOKA MCHEZAJI WA SUDAN. 


MASHABIKI WA TANZANIA WAKIJA KUWAPA SUPPORT TIMU YAO.
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania Bara, imeanza vema kampeni zake za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, baada ya kuichapa mabao 2-0 Sudan katika mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda.
Ushindi huo, unaiweza Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi B, nyuma ya Burundi inayoongoza kwa wastani wa mabao.
Hadi mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yote yakipachikwa kimiani na mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyetumia vema krosi za Mrisho Khalfan Ngassa.
Bocco alifunga bao la kwanza Bocco aliiwahi vema krosi ya Ngassa aliyewatoka mabeki wa Sudan wingi ya kushoto na kuitumbukiza kimiani dakika ya 14.
Adebayor wa Chamazi aliwainua tena vitini mashabiki wa Tanzania dakika ya 28, akiunganisha krosi ya Ngassa tena kutoka kule kule kushoto.
Kwa ujumla Tanzania Bara walicheza vizuri kipindi cha kwanza, wakishambulia zaidi kupitia pembeni, kulia Simon Msuva ambaye hakuwa na madhara sana na kushoto Ngassa ambaye alikuwa mwiba mchungu haswa kwa Wasudan.
Pamoja na Bara kutawala kipindi cha kwanza, lakini Wasudan walifanya mashambulizi kadhaa ya kushitukiza na sifa zimuendee mlinda mlango Juma Kaseja, ambaye alioko amichomo miwili ya hatari mno.
Kipindi cha pili Stars, inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen iliendelea kutawala mchezo, lakini safu ya ulinzi ya Sudan iligangamala.
Tanzania Bara; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar/Amri Kiemba, John Bocco, Mwinyi Kazimoto na Simon Msuva/Shaaban Nditi.
Sudan; Ebd Elrahman Ali, Moawia El Amin, Sami Abdallah, Faris Abdallah, Hamoda Bashir/Farid Mohamed, Mohamed El Mortada, Sadam Abutalib, Mohamed Mussa Idris, Modathir Mohamed, Adam Sayer/Osama El Rashid na Mohamed Osman/Saed Siddig.
Katika mchezo wa awali, Burundi walishinda mabao 5-1, mabao yake yakifungwa na Chris Nduwarugira dakika ya 35 na 88, Yussuf Ndikumana dakika ya 41 na Suleiman Ndikumana dakika ya 84 na 90, wakati la Somalia lilifungwa na Mohamed Jabril kwa penalti dakika ya 55.
Matokeo hayo yanalifanya Kundi B lizidi kuwa gumu, kwani Burundi inaongoza kwa pointi zake tatu na mabao mengi, Tanzania ya pili kwa pointi tatu na mabao mawili- lakini bado Sudan wanaweza kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo.
                    NENO LA LEO LANGU

MUNGU BARIKI TANZANIA MUNGU BARIKI WACHEZAJI WAKE.

Saturday, November 24, 2012


HABARI KUTOKA KAMPALA ZA KENYA NA UGANDA LEO HII TIMU YA UGANDA IMEWEZA KUIFUNGA TIMU YA KENYA KWA MABAO 1-0.
HABARI KUTOKA KAMPALA ZA KENYA NA UGANDA LEO HII TIMU YA UGANDA IMEWEZA KUIFUNGA TIMU YA KENYA KWA MABAO 1-0.

TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imelalamikia Uwanja mbovu wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, waliopelekwa kufanya mazoezi leo kujiandaa na mechi ya kesho ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge 2012 dhidi ya Sudan, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura amewasilisha malalamiko hayo kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rodgers Mulindwa ambaye ameahidi kuyafanyia kazi.
“Tutalifanyia kazi suala hilo, tutakuwa na kikao kesho litawasilishwa na litapatiwa usumbufu, mwanzo huwa na matatizo, lakini mambo yatakuwa mazuri,”alisema Mulindwa.
Hata hivyo, inashangaza Stars kupelekwa katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, wakati kwenye mpango wa awali kabisa wa FUFA ilitakiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nakawa.
Kwa upande wake, kocha wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesikitishwa na kutowasili kwa washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
“Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu hawajafika, lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.
“Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.
Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia 

Friday, November 23, 2012

UMOJA wa wanamichezo waliowahi kucheza klabu mbalimbali zikiwemo za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara wenye maskani yao mjini Bukoba, Kagera, Bukoba Veteran Sports Club ni katika kuhamasisha ushiriki wa timu za Tanzania, Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes, kwenye michuano ya Kombe la Tusker Challenge inayofanyika jijini Kampala Uganda, umeandaa safari ya mashabiki walioko mkoani humo Kanda ya Ziwa kwa ujumla kwenda kushangilia mechi za timu hizo.Katibu Mkuu wa Bukoba Veterans, Shijja Richard ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba kwa kuanzia, mashabiki hao wataondoka mjini Bukoba Jumapili Novemba 25, 2012 kwenda kuishangilia timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo dhidi ya Sudan Kaskazini.Amesema nia na madhumuni ya safari hiyo ni kuhamasisha wachezaji wa timu za taifa za Tanzania waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kutoa hamasa kwa watanzania kujenga tabia ya kushangilia timu zao na pia wanadhani kuwa ushiriki wao utaongeza ushindani katika michuano hiyo.Amesema tayari taratibu zote zimeshafanyika ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) ili wawasiliane na mamlaka zinazohusika kwa ajili ya kupatiwa eneo maalumu uwanjani litakalowezesha watanzania waweze kuishangilia vizuri timu ya taifa.
“Tunatarajia kwenda uwanjani na zaidi ya mashabiki 60 ambao hivi sasa wanakamilisha taratibu za mwisho za kuvuka mpaka wa nchi. Matarajio yetu ni kuendelea kuziunga mkono timu za taifa katika michuano hiyo hadi kufikia mwisho wa michuano. Tunaomba watanzania wengine walioko kanda ya ziwa katika mikoa ya Shinyanga, Mara na Mwanza watuunge mkono,”alisema Richard.Kikosi cha kinatarajiwa kuwasili leo mjini Kampala, kikitokea Mwanza tayari kwa mashindano hayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Tusker Challenge 2012 yanayotarajiwa kuanza kesho.Stars imekuwa kambini mjini Mwanza kwa takriban wiki mbili sasa ikijifua vikali chini ya kocha wake, Mdenmark Kim Poulsen kujiandaa kwenda kutwaa taji la nne la Challenge.Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichopo kambini mjini Mwanza, kinaundwa na makipa; Juma Kaseja (Simba SC) na Deogratius Mushi ‘Dida’ wa Azam FC, mabeki; Kevin Yondan (Yanga), Erasto Nyoni (Azam FC), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Shomari Kapombe na Amir Maftah (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo (Yanga) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar) wakati washambuliaji ni John Bocco ‘Adebayor’ (Azam FC), Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa (TPM, DRC).Bara ambayo inajivunia kutwaa mara tatu Kombe la Challenge katika miaka ya 1974, 1994 na 2010 na kushika nafasi ya pili mara tano, imepangwa Kundi B pamoja na Sudan, Burundi na Somalia.
Itaanza kampeni zake Novemba 25 kwa kumenyana na Sudan saa 12:00 jioni, mchezo utakaotanguliwa na mechi kati ya Burundi na Somalia itakayoanza saa 9:00 Alasiri kabla ya kurudi tena dimbani, Novemba 28 kukipiga na Burundi, mchezo utakaotanguliwa na mechi kati ya Somalia na Sudan.Stars iatahitimisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Somalia Desemba 1, mchezo utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Sudan na Burundi. Mechi zote za Stars zitakuwa saa 12:00 jioni.
MAKUNDI RATIBA TUSKER CHALLENGE 2012:KUNDI A: Uganda, Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini
KUNDI B: Tanzania, Sudan, Burundi na Somalia
KUNDI C: Malawi, Eritrea, Rwanda na Zanzibar
RATIB KUNDI A:Novemba 24, 2012:
Ethiopia v Sudan (Saa 9:00 Alasiri)Uganda v Kenya (Saa 12:00 jioni)Novemba 27, 2012:
Sudan Kusini v Kenya (Saa 9:00 Alasiri)Uganda v Ethiopia (Saa 12:00 jioni)Novemba 30, 2012:
Kenya v Ethiopia (Saa 9:00 Alasiri)Sudan Kusini v Uganda (Saa 12:00 jioni)
RATIBA KUNDI B:Novemba 25, 2012:
Burundi v Somalia (Saa 9:00 Alasiri)Tanzania v Sudan (Saa 12:00 jioni)Novemba 28, 2012:
Somalia v Sudan (Saa 9:00 Alasiri)Tanzania v Burundi (Saa 12:00 jioni)Desemba 1, 2012:
Sudan v Burundi (Saa 9:00 Alasiri)Somalia v Tanzania (Saa 12:00 jioni)
RATIBA KUNDI C:Novemba 26, 2012:
Zanzibar v Eritrea (Saa 9:00 Alasiri)Rwanda v Malawi (Saa 12:00 jioni)Novemba 29, 2012:
Malawi v Eritrea (Saa 9:00 Alasiri)Rwanda v Zanzibar (Saa 12:00 jioni)Desemba 1, 2012:
Malawi v Zanzibar (Saa 9:00 Alasiri)Eritrea v Rwanda (Saa 12:00 jioni)
ROBO FAINALI:Desemba 3, 2012Mshindi Kundi C vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa 10:00 jioni)Mshindi Kundi A vs Mshindi wa Tatu Bora wa pili (Saa 1:00 usiku)Desemba 4, 2012 (16:00):
Mshindi Kundi B vs Mshindi wa Tatu Bora wa kwanza (Saa 10:00 jioni)Mshindi wa Pili Kundi A vs Mshindi wa Pili Kundi C (Saa 1:00 usiku)
NUSU FAINALI:
Desemba 6, 2012Nusu Fainali ya Kwanza (Saa 10:00 jioni)Nusu Fainali ya Pili (Saa 1:00 usiku)
MSHINDI WA TATU:
Desemba 8, 2012Waliofungwa Nusu Fanali (Saa 10:00 jioni)
FAINALI:
Desemba 8, 2012Walioshinda Nusu Fainali (Saa 1:00 usiku)

x



MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara huko mashakani kufanyika baada ya Mapato ya Taifa(TRA) kuzifunga akaunti za udhamini wa ligi hiyo.
TRA ilizifunga akaunti za TFF ikiwemo ya udhamini wa ligi hiyo ikiwa ni sehemu ya kulishinikiza Shirikisho la Soka nchini(TFF) kulipa makato ya kodi kwenye mishahara ya timu ya taifa(Taifa Stars) tokea kipindi cha kocha Marcio Maximo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini(TFF) Sunday Kayuni alisema mishahara ya makocha wa Taifa Stars tangia kocha Marcio Maximo ilikuwa haikatwi kodi na hivyo kufanya gharama wanazodaiwa na mamlaka ya Mapato kufikia shilingi milioni 157,407.968.00.
Alisema wamekuwa wakipata taarifa ya mara kwa mara toka TRA ikiwakumbusha juu ya makato hao na wao kuwajibu kuwa hawahusiki kwenye malipo ya mishahara ya makocha hao kwani ni waajiriwa wa Serikali.
Kayuni alisema hata hivyo kwa kuwa wao ndio walezi wa makocha hao TRA imeamua kuzifunga akaunti zao ikiwemo ya udhamini wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara ambayo ina zaidi ya shilingi milioni 300.
Alisema kutokana na hali hiyo walifanya mazungumzo ya mara kwa mara na TRA bila ya mafanikio na kuamua kuunda kamati itayoshirikisha Kamati ya Ligi ikishirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na mamlaka hiyo ya mapato nchini.
“Tunaona labda tukiunganisha nguvu zetu labda wenzetu wa TRA wanaweza kutusikiliza, hivyo Kamati tutakayounda kwa kushirikiana na wizara itakwenda kujaribu kufanya tena mazungumzo na TRA.”alisema Kayuni.
Kwenye Mkutano huo na waandishi wa habari Kayuni aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi Kuu Saidi Mohamedi na Mkurugenzi Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara Silas Mwakibinga, ambao wote walionyesha umuhimu wa kuunganisha nguvu zao kuishawishi TRA.



MAMBO yameiva Yanga- matumaini ya wapenzi wa klabu hiyo kushuhudia klabu yao ikiwa na Uwanja mpya wa kisasa yameanza kuonyesha dalili za kutimia, kufuatia uongozi wa klabu hiyo kusaini makubaliano ya awali na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group iliyojenga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Kaunda.Mwenyekiti wa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, Alhaj Yussuf Mehboob Manji leo amesaini makubaliano na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, David Zhang, makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga, Dar es Salaam.Katika makubaliano hayo, ujenzi huo wa Uwanja utakaokuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 30,000 hadi 40,000 utaanza rasmi Juni mwakani.Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kusaini makubaliano hayo leo mchana, Alhaj Manji alisema kwamba wanfurahi kuanza safari ya ujenzi wa Uwanja wao na anaamini huo ni mwanzo wa mzuri wa mipango yao ya kuifanya Yanga ijitegemee kiuchumi.Katika hatua nyingine, Manji amesema kwamba katika mipango yao ya kuifanya Yanga ijimudu kiuchumi, wanafikiria kulikarabati pia jengo dogo la klabu hiyo, liliopo Mtaa wa Mafia.Alhaj Manji alisema Jumatatu kampuni hiyo ya ujenzi kutoka China, ambayo ndiyo iliyojenga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itachukua vipimo kwenye Uwanja wa Kaunda na Uongozi wa Yanga kuliwasilisha suala la ujenzi huo kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu hiyo, Desemba 8, mwaka huu.Alisema baadhi ya fedha kwa ajili ya uwanja huo wa kisasa watakapo benki na gharama nyingine zitatokana na michango ya wanachama baada ya kuwa wamepata gharama nzima za ujenzi za uwanja huo.Meneja Mkuu wa Kampuni ya Beijing Cobnstruction Engineering Group alisema wanafurahia kufikia makubaliano ya awali ya ujenzi wa uwanja na klabu ya Yanga.Alisema wao ndio walijenga Uwanja wa Taifa na viwango vya ujenzi vya uwanja huo vilisifiwa na timu ya taifa ya Brazil iliyokuja kucheza mechi ya kirafiki na Tanzania mwaka 2010 ikiwa njiani kuelekea Afrika Kusini ambako fainali za kombe la Dunia zilifanyika.


Sunday, November 11, 2012


PICHA ZA SIMBA SPORT CLUB NA TOTO AFRICAN JANA WALIVYOBANWA SIMBA KATIKA UWANJA WA DAR-ES -SALAAM,TOTO AFRICAN WAKI UBUKA NA USHINDI WA 1-0.